Njia mpya ya kupanga na kusimamia Pesa


Fanikisha malengo yako kwa kutumia App bora zaidi ya Kibenki.

Simamia pesa kwa ufanisi ili ufanikishe malengo yako muhimu

Weka Malenga yako

Watu wote makini wana malengo maalumu ya kifedha. Tembo inakuwezesha kutengeneza malengo yako binafsi, na inakusaidia kutunza pesa ili uyafanikishe.

Angalia Maendeleo yako

Tembo itakupa notification na kukutumia jumbe mara kwa mara ili uweze kuona maendeleo ya malengo yako. Tembo itakuwezesha kuwa na picha kamili ya akiba zako na balansi zako muda wote.

Jipatie Riba na Faida

Pesa zako zinatunzwa na benki mshirika wetu kwenye akaunti inayotoa riba kubwa. Lengo letu ni kutunza pesa zako kwa usalama, lakini pia kuhakikisha inapata riba ili ikusaidie ufikie malengo yako mapema

App yetu ni bora kuliko ya benki yoyote, Ijaribu!


Hatua Rahisi, lakini Matokeo makubwa

Weka malengo yako ya kifedha

Unaweza kutengeneza malengo zaidi ya moja, zingatia mambo muhimu unayotaka kufanikisha

Weka njia ya kuingiza pesa

Unaweza kuweka pesa kwenye malengo yako kwa mitando ya simu, au kwa njia za kibenki.

Soma notification kwenye App

App itakutumia notification na jumbe kukumbusha na kukupa taarifa kuhusu balansi, miamala na malengo yako.

Fanya uwekezaji

Baadaye, utaweza kufanya uwekezaji ili fedha zako zipate kukua zaidi ili ufikie malengo yako mapema

Weka Pesa Moja kwa Moja

Ukiunganisha akaunti yako ya benki ya mshahara, utaweza kuweka pesa kwenye malengo yako automatically.

Pata Mikopo

*Inakuja hivi karibuni* Utaweza kupata mikopo endapo utapata dharura au una lengo maalumu linalostahili kupata mkopo.

F.A.Q

Majibu ya maswali muhimu

Tembo imeingia mkataba na Benki ambayo ndiyo inayotunza pesa zako kwa usalama. Unapoanza kutumia App ya Tembo, tunakufungulia akaunti ya benki kwa jina lako na hii akaunti ndiyo inayopokea na kutunza pesa zako. Huduma hii pamoja na benki zinasimamiwa na benki kuu ya Tanzania, na hivyo kutunza pesa kutumia App ya Tembo ni salama kama tu kuweka pesa kwenye akaunti yako ya benki.

Ndiyo, Tembo imeingia mkataba na Benki ambayo ndiyo inayotunza pesa zako kwa usalama. Unapoanza kutumia App ya Tembo, tunakufungulia akaunti ya benki kwa jina lako na hii akaunti ndiyo inayopokea na kutunza pesa zako. Tembo imeingia mkataba ambao unahakikisha kwamba akaunti hii inapata riba. Ukiingia kwenye App yako ya Tembo, utaona kiasi cha riba ambacho balansi yako inapata kila siku.

Lengo letu ni kukuwezesha kufikia malengo yako muhimu ya kifedha. Tunaamini kutunza pesa kwa nidhamu ni jambo muhimu sana ili ufanikishe malengo yako, hivyo tunakuwezesha kuweka malengo maalumu ya mambo unayataka kuyafanikisha. Ndani ya App ya Tembo, utaweza kutengeneza malengo yako kwa urahisi sana.

Unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye malengo yako. Wakati unajiunga na Tembo, utapewa nafasi ya kuunganisha akaunti yako ya Benki kama unayo ili uweke pesa moja kwa moja. Kama hauna akaunti ya benki, utaweza kuweka pesa kwa kutumia Huduma za simu kama TigoPesa, Mpesa, Airtel Money nk..

Unapoanza kutumia huduma za Tembo, inatubidi tukutengenezee akaunti kwenye benki mshirika wetu ili tuweze kutunza pesa zako kwa usalama. Hivyo, inatubidi tupate taarifa zako zinazotosheleza kufungua akaunti yako ya benki. Taarifa zote tunazoomba ni zile ambazo Benki kuu na serikali inahitaji wateja wote wa benki wawe nazo, hii inajumlisha pia kitambulisho chako na picha yako. Taarifa hizi ni muhimu pia kwa sababu zitakusaidia wewe au ndugu zako waweze kupata fedha zako hata kama umepoteza simu, au umeshindwa kuingia kwenye App kwa sababu moja au nyingine.

Taarifa zote tunazokusanya zinatumika tu kwa makusudi ya kukupa wewe huduma zetu. Taarifa zako zinatunza kwa njia salama na hatua madhubuti zinachukuliwa na zitazidi kuchuliwa kuzuia watu wasiohusika kuzipata. Washirika wetu wote ni taasisi zinazotambuliwa na serikali na zinafuata sheria zote za usiri na ulinzi wa taarifa.

Hatuoni wala hatuna njia ya kuona password zako za mitandao ya simu. Hatukusanyi wala hatutunzi taarifa zako za kadi za malipo kwa sababu malipo ya kadi yanafanywa na mtoa huduma za malipo ambaye amepewa leseni na amepitishwa na PCIDSS.

Contact

Wasiliana Nasi

Anuani

United States

447 Broadway,
2nd Floor Suite #1528,
New York,
NY 10013


Tanzania

204 Abla Complex,
Rose Garden Road,
Mikocheni,
Dar es Salaam,TZ.

Namba za Simu

+255 659 966 692

+44 7741915289

Barua Pepe

info@temboplus.com
victor@temboplus.com

Masaa ya kazi

Monday - Friday
9:00AM - 05:00PM